Nyota wawili wa Yanga Celestine Ecua na Lassine Kouma ni sehemu ya kikosi cha Tchad kinachojiandaa na mechi za kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia 2026
Ecua na Kouma wamejumuishwa katika timu ya Taifa ya Tchad baada ya kubadili uraia kutoka nchi zao za awali
Ecua alikuwa raia wa Ivory Coast wakati Kouma alikuwa raia wa Mali wote wakiwa na wazazi wenye asili ya Tchad
Tayari Ecua ameitumikia Tchad katika mchezo uliopita dhidi ya Ghana akifunga bao lililowapa matokeo ya sare
Yawezekana katika kikosi cha Yanga wameanza taratibu lakini hakuna shaka juu ya vipaji vya nyota hawa

ADVERTISE HERE