Baada ya Serikali kusitisha matumizi ya uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mechi za ligi kuu, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea dimba la KMC Complex
Uwanja wa Benjamin Mkapa unaingia katika awamu nyingine ya ukarabati hivyo kuzilazimu klabu za Yanga na Simba ambazo awali ziliruhusiwa kutumia uwanja huo, kutafuta viwanja vingine
Msimu uliopita Yanga ilianzia uwanja wa Azam Complex lakini baadae ikahamia KMC Complex ambako walifanikiwa kushinda mechi zote walizocheza katika uwanja huo
Yanga ilicheza mechi moja ya ligi katika uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Pamba Jiji Wananchi wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0
Mechi za Kimataifa zinaweza kuendelea kupigwa dimba la Mkapa au kupelekwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar
ADVERTISE HERE