Yanga imekamilika sasa

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
1 Aug 2017
Yanga imekamilika sasa
Wakati dirisha la usajili linafunguliwa mwezi Juni mashabiki wa Yanga walikuwa na wakati mgumu sana kutokana na 'mkwara' uliokuwa unapigwa na wale wa upande ulee.

Wao kwa haraka walisajili wachezaji watatu kwa mpigo kutoka klabu ya Azam FC huku sisi tukidaiwa 'kupokwa' wachezaji kutokana na ukata.

Wachezaji kama Waziri Junior, Mbaraka Yusuph na Salmini Hoza walikuwa wakihusishwa na Yanga lakini eti ikadaiwa tumeshindwa kuwasajili kwa sababu hatuna fedha.

Tena baadhi ya magazeti yakafika mbali kuidhalilisha timu yetu kuwa baadhi ya wachezaji (Hoza) wamerejesha kishika uchumba cha Yanga na kusajiliwa timu nyingine.

Abdalla Shaibu 'Ninja' na Pius Buswita ni wachezaji pekee ambao tulifanikiwa kuwasajili wakati huo licha ya kebehi kibao kutoka kwa mahasimu wetu waliokuwa wameteka vyombo vyote vya habari za michezo.

Hofu ikaanza kuwajaa pale ilipotangazwa tumefanikiwa kumsajili Ibrahim Ajib. Wapo ambao hawakuamini, lakini siku alipotambulishwa habari ikawa tofauti.

Aidha kuondoka kwa Niyonzima nako hakukutuacha salama.

Matusi yaleyale ya ukata yakaporomoshwa. Kumbe maskini hawakujua kuwa ni Yanga iliyokuwa imeamua kuachana nae baada ya kutathmini kiasi cha pesa alizotaka alipwe na uwezo wake kwa sasa.

Lakini siku Yanga ilipotangaza kumuongezea mkataba Donald Ngoma ndio siku ambayo wale wa upande wa kule 'waliufyata'

Waliamini wataweza kumsajili Ngoma kwa kuwa Yanga 'salio limekata' mmoja wa viongozi wa Kamati yao ya usajili aliwahi kusema hivyo.

Hawajakaa sawa, wakasikia Amissi Tambwe nae ameongezwa mkataba wa miaka miwili, hapo ndipo upole ulipowaingia.

Baadae wakaja Youthe Rostand, Ramadhani Kabwili na Burhani Akilimali wachezaji wenye viwango vya juu sana licha ya kutokuwa na majina makubwa.

Niwaambie siku aliyotua Papi Kabamba Tshishimbi ndiyo sikua ambayo wale jamaa walipagawa.

Wanamjua Tshishimbi na walijaribu kumsajili kabla ya Yanga lakini hawakufanikiwa. Hili jembe litatuliza kabisa kiungo cha Yanga.

Hatukatai Niyonzima alikuwa mzuri kwenye kuchezesha timu lakini alikuwa mbovu sana kwenye kukaba, huyu Tshishimbi ana sifa zote.

Ana pumzi, anapora mipira na anapiga pasi za maana! Hapa wapinzani wajiandae tu.

Haya jana imetambulishwa mashine nyingine Rafael Daudi kutoka Mbeya City. Kama kawaida yao huyu nae walijaribu kumrubuni aende upande wao, ikashindikana.

'Mido' hii ni habari nyingine mbaya kuisikia. Licha ya kuwa mzuri kwenye kuchezesha timu, kiungo huyu ni mpachika mabao mzuri sana.

Nakiri, akiwa Mbeya City Daudi aliwazidi viungo wetu kwa idadi ya mabao kwa msimu miwili mfululizo. Msimu wa 2015/16 alifunga mabao nane na akafanya hivyo msimu uliomalizika.

Yanga hii haijawahi kutokea, viongozi wetu waliosimamia zoezi la usajili wakiongozwa na Mwenyekiti Hussein Nyika wanastahili kupongezwa.

Mwalimu Lwandamina atakuwa na kazi ngumu ya kupanga kikosi cha kwanza kutokana na uwezo mkubwa wa wachezaji waliosajiliwa.

Yanga imekamilika kila idara, kuanzia golini mpaka washambuliaji.

Ebu fikiri, timu yenye Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib inaweza isitwae ubingwa kwa msimu wa nne kweli?

Timu yenye viungo Thabani Kamusoko, Papi Kabamba Tshishimbi, Rafael Daudi na Pius Buswita inashindwaje?

Kwenye ulinzi kuna ongezeko la wachezaji wawili wa maana. Unaambiwa kuna Mnigeria anapiga miguu yote, na anapiga vichwa balaa. Kona zote mabao...!

Licha ya kuondoka Msuva Yanga bado ina washambuliaji wa pembeni mahiri. Emanuel Martini, Godfrey Mwashiuya, Burhani Yahaya, Juma Mahadhi na Yusuph Mhilu.

Hawa vijana wana vipaji vya hali ya juu na kutakuwa na ushindani wa namba baina yao msimu huo, jambo litakalofanya waboreshe viwango vyao.

Kazi kwao...!
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’