Dimba la Mkapa kufungwa miezi sita

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2025
Dimba la Mkapa kufungwa miezi sita

Klabu za Yanga na Simba SC, zitalazimika kutafuta viwanja mbadala kwa michezo yao ya Ligi Kuu ya Bara na michuano ya kimataifa kufuatia uthibitisho wa serikali kuhusu kufungwa kwa miezi sita kwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya ukarabati mkubwa.

Uwanja huo wa kitaifa wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 60,000, ambao umekuwa uwanja wa nyumbani kwa timu zote mbili msimu huu baada ya kuhamia kutoka Uwanja mdogo wa KMC Complex, unatarajiwa kufanyiwa marekebisho makubwa ya nyasi kuanzia mwezi huu.

Yanga tayari wamecheza mechi dhidi ya Wiliete FC ya Angola kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Pamba Jiji FC kwenye ligi katika uwanja huo, huku Simba wakipambana na Fountain Gate FC na Namungo FC kwenye ligi, pamoja na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Gaborone United ya Botswana.

Ratiba rasmi ya CAF inaonyesha kuwa Yanga wanatarajiwa kuikaribisha Silver Strikers ya Malawi katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa tarehe 25 Oktoba, wiki moja baada ya mchezo wa kwanza mjini Lilongwe.

Wapinzani wao wakubwa, Simba, wanatarajiwa kuikaribisha Nsingizini Hotspurs ya Eswatini kwenye uwanja huo huo tarehe 26 Oktoba, baada ya mchezo wa awali tarehe 18 Oktoba. Hata hivyo, mechi hizi sasa zipo shakani kulingana na tarehe rasmi ya kuanza kwa ukarabati.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amethibitisha kuwa kufungwa kwa uwanja huo kunahusu vilabu vyote viwili.

“Mechi ya mwisho ya ligi iliyochezwa Benjamin Mkapa ilikuwa kati ya Simba na Namungo. Baada ya hapo kazi ya ukarabati inaanza rasmi. Ukarabati utafanyika kwa muda wa miezi sita,” alisema Msigwa.

“Uwanja utapatikana tu kwa michezo ya kimataifa iwapo muda hautagongana na kazi za ukarabati. Endapo ukarabati utakuwa umeanza, hata michezo ya CAF italazimika kuhamishwa.”

Aidha, ili kupunguza usumbufu, serikali tayari imependekeza viwanja mbadala.

“Tunao Uwanja mpya wa Amaan kule Zanzibar na Uwanja wa Azam Complex huko Chamazi. Itakuwa juu ya vilabu kuamua,” alifafanua Msigwa.

Akaongeza kuwa suluhisho la muda mrefu ni Uwanja wa Uhuru, ambao kwa sasa nao uko kwenye ukarabati na unatarajiwa kufunguliwa tena tarehe 21 Novemba.

“Uwanja wa Uhuru utawekewa nyasi bandia za ubora wa juu zilizoidhinishwa na CAF na FIFA. Baada ya kukamilika, utaweza kuwa mwenyeji wa michezo ya kimataifa na ya CAF,” alibainisha.

Kufungwa kwa Uwanja wa Benjamin Mkapa ni pigo kwa Yanga na Simba, ambazo zimekuwa zikifurahia sapoti kubwa ya mashabiki wao kwenye uwanja huo.

Kwa michezo muhimu ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayokaribia, vigogo hao wa Tanzania sasa wanakabiliwa na changamoto ya kuchagua viwanja vipya vya muda.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
18m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’