Folz kikaangoni Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2025
Folz kikaangoni Yanga

Kocha mkuu wa Yanga SC, Romain Folz, sasa yupo katika kipindi kigumu zaidi tangu ajiunge na Wananchi.

Baada ya sare tasa dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, hatma yake ipo mikononi mwa mabosi wa klabu hiyo ambao wameanza kuhoji uwezo wake wa kuipeleka timu mbele.

Awali, uongozi wa Yanga ulionekana kumpa Folz uhakika wa nafasi yake, lakini matokeo ya suluhu jijini Mbeya yamebadili upepo. Kuna taarifa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya utendaji wameonyesha wasiwasi juu ya uwezo wake kubadilika kimbinu na kushinda michezo yenye mazingira magumu.

Hoja ya "changamoto ya uwanja wa Sokoine" imeonekana kutowashawishi mabosi hao wa Yanga. Wamekumbusha namna timu hiyo ilivyofanya vizuri msimu uliopita katika mazingira hayo hayo, ikiwemo ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Tanzania Prisons mkoani Mbeya.

Imeonekana sare dhidi ya Mbeya City si kigezo cha kupunguza matarajio, bali ni dalili za changamoto kubwa kimbinu.

Kuna kila dalili kuwa uongozi wa Yanga unaweza kufanya uamuzi mgumu, ikiwemo kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi endapo hali haitabadilika mapema. Hii inatokana na presha kubwa ya mashabiki pamoja na matarajio ya timu hiyo kufanya vyema ndani na nje ya Tanzania.

Tangu msimu huu uanze, Folz ameiongoza Yanga kwenye mechi tano za mashindano, akishinda michezo minne na kutoka sare mmoja. Hata hivyo, licha ya rekodi hiyo nzuri, mashabiki wamelalamikia aina ya uchezaji wa timu yao, wakidai hauna ubunifu na hauendani na hadhi ya mabingwa watetezi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’