Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua ameishukuru klabu hiyo baada ya kupata nafasi ya kuitwa timu ya Taifa ya Ivory Coast inayokabiliwa na mechi mbili za kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Shelisheli na Kenya
Pacome ni mchezaji pekee anayecheza Afrika ambaye amejumuishwa katika kikosi cha Ivory Coast kilichosheheni mastaa wanaocheza barani Ulaya na Asia
Aliitwa kwa mara ya kwanza msimu wa 2023/24 lakini hakupata nafasi ya kucheza akiwa ni majeruhi lakini wakati huu amejumuishwa akiwa yuko 'fit' na pengine atapata nafasi ya kucheza
"Nina furaha sana, naenda kucheza timu ya Taifa ya Ivory Coast, nimeitwa kucheza mechi mbili za kufuzu kombe la Dunia, niwashukuru sana mashabiki wa Yanga, Rais na wafanyakazi wote wa benchi la ufundi kwa kazi yenu iliyotukuka"
"Ninakwenda kuiwakilisha klabu kubwa ya Yanga, nina furaha sana kwa wito huu katika timu ya Taifa, ninawashukuru sana mashabiki wa Yanga kwa kuniunga mkono," alisema Pacome
Katika mchezo dhidi ya Kenya, Pacome atakutana uso kwa uso na Duke Abuya ambaye amejumuishwa katika kikosi cha Bennie McCarthy