Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua amejumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026
Ivory Coast itacheza mechi mbili Oktoba 10 dhidi ya Shelisheli na Oktoba 14 dhidi ya Kenya
Kiwango kikubwa anachoonyesha katika kikosi cha Yanga tangu msimu uliopita hatimaye kimelipa kwani anakuwa miongoni mwa wachezaji wachache wanaocheza Afrika ambao wamejumuishwa kikosi cha Ivory Coast
Hii ni mara ya pili Pacome anajumuishwa kikosi cha Ivory Coast tangu aliposajiliwa na Yanga akitokea Asec Mimosas misimu miwili iliyopita

ADVERTISE HERE