Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto amerejeshwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kitakachoingia kambini Oktoba 04 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Zambia ambao utapigwa Oktoba 08
Aidha kocha wa Stars Hemed Morocco pia amewajumuisha kwa mara ya kwanza Aziz Andabwile, Israel Mwenda na Offen Chikola katika kikosi chake
Pia wamo mabeki wa kati Dickson Job na Ibrahim Bacca ambao wameendelea kuwa tumaini la Stars kwenye safu ya ulinzi

ADVERTISE HERE