Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube amerejeshwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Zimbabwe kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu kombe la Dunia 2025 ambazo zitapigwa kuanzia mwishoni mwa wiki
Dube anaungana na mastaa wengine wa Yanga ambao tayari wamepokea wito kwa ajili ya kuzitumikia timu za Taifa
Nyota hao ni Duke Abuya (Kenya), Moussa Balla Conte (Guinea), Djigui Diarra (Mali) na Celestin Ecua (Chad)
Aidha kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Hemed Morocco ametangaza kikosi chake kitakachoikabili Zambia Oktoba 08 katika mchezo wa kuhitimisha raundi ya 8
Ibrahim Bacca, Dickson Job, Aziz Andabwile, Israel Mwenda, Offen Chikola na Bakari Mwamnyeto wamejumuishwa katika kikosi hicho
Clement Mzize amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Morocco lakini amekosekana akiendelea kuuguza majeraha ya nyama za paja