Folz ameuona ukubwa wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Oct 2025
Folz ameuona ukubwa wa Yanga

Mkufunzi wa Yanga Romain Folz bila shaka aliona ukubwa wa timu hiyo mkoani Mbeya baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City uliopigwa dimba la Sokoine

Folz kwa mara ya kwanza alikutana na presha ya kuwa kocha wa Yanga baada ya mchezo huo uliomalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Pengine alikuwa na safari ndefu kutoka uwanjani hadi vyumba vya kubadilishia nguo mamia ya mashabiki wakipaza sauti zao kuonyesha kutoridhishwa jinsi timu yao inavyocheza

Baada ya kuisimamia Yanga katika mechi nne zilizopita ambazo zote alishinda, jana ilikuwa mara yake ya kwanza kuiongoza Yanga mkoani ambapo alishuhudia dimba la Sokoine likiwa 'full-house'

Folz amesisitiza kuwa kutocheza vyema kwa timu yake katika mchezo huo kulichangiwa na hali isiyoridhisha ya uwanja wa Sokoine

Baada ya presha ya mashabiki kwa uongozi wa Yanga kutaka mabadiliko yafanyike katika benchi la ufundi, Meneja wa habari na mawasiliano Ali Kamwe amewataka mashabiki wawe watulivu kwani viongozi wao ni wasikivu na watafanya maamuzi kwa kuzingatia maslahi mapana ya klabu

Tetesi kutoka ndani ya uongozi zimedokeza kuwa wakati ligi ikisimama kupisha kalenda ya FIFA, uongozi unatarajiwa kukutana na benchi la ufundi kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwenendo wa timu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’