Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kufikia tamati Jumatatu May 28 kwa timu zote nane kushuka dimbani katika viwanja tofauti.
Lakini kabla ya Jumatatu, kesho Ijumaa Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kuhitimisha michezo yake ya kiporo itakapoikaribisha Ruvu Shooting.
Yanga imepata ushindi wake wa kwanza juzi baada ya kuchezo michezo tisa kwa kuilaza Mbao FC bao 1-0.
Katika mchezo huo Yanga ilionekana kuimarika zaidi na ingeweza kuvuna kalamu ya mabao kama washambuliaji wake wangekuwa makini.
Kaimu Kocha wa Yanga, Noel Mwandila amesema ushindi dhidi ya Mbao FC umeongeza hamasa na kujiamini kwa kikosi chake na sasa wanasaka ushindi kwenye michezo miwili iliyobaki dhidi ya Ruvu Shooting na Azam FC.
Kikosi cha Yanga kinajifua kwenye uwanja wa Polisi, Kilwa kikiwa chini ya Mwandila na Nsajigwa.
Kocha Mkuu Mwinyi Zahera bado hajarejea kutoka DR Congo alikokwenda kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa.
DR Congo inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria May 28.

ADVERTISE HERE