Lipuli ilikusudia kumpeleka Salamba Simba/Azam

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 May 2018
Lipuli ilikusudia kumpeleka Salamba Simba/Azam
Uongozi wa Lipuli FC umesema uko tayari kumuuza mshambuliaji wake Adam Salamba kama itapokea ofa isiyo chini ya Mil 50.

Mwenyekiti wa Lipuli FC Ramadhani Mahano amesema tayari wamepokea ofa mbili kutoka kwa vilabu vya Simba na Azam FC na wamewaelekeza juu ya masharti yao hayo.

Salamba alitakiwa kwa mkopo na klabu ya Yanga na ikiwezekana asajiliwe kabisa ili aweze kutumika kwenye michuano ya kombe la Shirikisho lakini Lipuli FC ilikataa maombi hayo ikieleza sababu ni kuwa kanuni za TFF, CAF na FIFA haziruhusu mchezaji kucheza zaidi ya timu mbili ndani ya msimu mmoja.

Lakini kama Lipuli wangemruhusu Yanga ingeweza kumtumia kwa kutumia kanuni hizo hizo kwa kuwa msimu wa VPL unamalizika Jumatatu May 28 na kama ni kuanza kuitumikia Yanga Salamba angeanza mwezi wa saba wakati huo usajili wa msimu mpya ukiwa tayari umefunguliwa.

Kimsingi hapa inaonekana wazi Lipuli ilikumbana na presha kutoka kwa timu za Simba/Azam zilizokuwa zinamtaka mchezaji huyo.

Wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Yanga TV hivi karibuni, Salamba alisema yeye yuko tayari kuitumikia Yanga, tatizo limekuwa upande wa viongozi wa Lipuli FC.

Mchezaji huyo anaeleza kuwa bado na mkataba katika klabu hiyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’