Leo Jumamosi majira ya saa 11 jioni Wananchi wana jambo lao pale uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa raundi ya pili hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Wiliete SC
Yanga itashuka katika mchezo huo bila ya mshambuliaji wake ghari zaidi kwa sasa Clement Mzize ambaye ni majeruhi
Mzize alipata majeraha wakati wa michuano ya CHAN ambapo katika mchezo uliopita uliopigwa Angola alitonesha majeraha hayo
Mshambuliaji huyo ambaye Yanga ilifanya kazi ya ziada kumbakisha kwenye dirisha la usajili kutokana na ofa nyingi zilizotua Jangwani, pia alikosekana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji
Huenda katika nafasi yake mkufunzi wa Yanga Romain Folz akamtumia Edmund John ambaye amefanya vyema kwenye mechi mbili zilizopita
Edmund aliifunga moja ya mabao ya Yanga kwenye ushinda wa mabao 3-0 ambao Yanga iliupata katika mchezo wa mkondo wa kwanza nchini Angola