Mfumo umetiki! kazi wanayo Wiliete SC leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Sep 2025
Mfumo umetiki! kazi wanayo Wiliete SC leo

Leo Jumamosi saa 11 jioni, macho yote ya mashabiki wa soka Tanzania yatakuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo Young Africans SC (Yanga) wataikabili Wiliete SC ya Angola katika mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Kauli mbiu ya “Mfumo umetiki” ndio dira ya Wananchi kuelekea mchezo huu. Kocha Romain Folz anaamini kikosi chake kimeiva na wachezaji wake watatekeleza kwa ufanisi mfumo anaoutaka.

Ushindi wa mabao 3-0 walioupata ugenini Angola unawapa nafasi kubwa ya kutinga Raundi ya Kwanza, lakini Yanga wamesisitiza watashambulia hadi mwisho ili kutinga hatua inayofuata kwa kishindo.

Mashabiki wa Yanga wanatarajiwa kufurika dimba la Mkapa leo na kuwa chanzo cha morali kubwa kwa kikosi chao. Nguvu ya nyumbani imekuwa ngao ya Wananchi mara kwa mara, na leo itakuwa jukwaa la kuthibitisha ubabe wao.

Iwapo Wananchi watakamilisha kazi yao leo, watasubiri mshindi kati ya Silver Strikers ya Malawi na Elgeco Plus ya Madagascar, waliotoka sare ya 1-1 katika mkondo wa kwanza. Mchuano wa marudiano nchini Malawi leo utaamua mpinzani anayefuata.

Kwa Yanga, malengo ni makubwa zaidi ya hatua ya awali, huu ni mwanzo wa safari ya kufika hatua ya makundi na hata kupiga hatua zaidi kwenye michuano hii mikubwa ya Afrika.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’