Kiungo mshambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli jana alipata tuzo yake ya kwanza msimu huu akiibuka nyota wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa
Maxi alifunga bao la pili la Yanga katika mchezo huo ambao Wananchi walianza vyema kampeni ya kutetea ubingwa wao wakishinda mabao 3-0
Mcongomani huyo ameendeleza pale alipoishia msimu uliopita akifunga bao katika mechi ya kwanza ya msimu kama alivyofanya msimu uliopita

ADVERTISE HERE