Msimu uliopita Yanga ilianzia msimu ugenini kule Kagera ikiumana na Kagera Sugar katika mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0
Maxi Nzengeli na Clement Mzize walifunga mabao ya Yanga katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Kaitaba
Msimu huu Wananchi wanaanzia uwanja wa nyumbani, Benjamin Mkapa wakiumana na Pamba Jiji mchezo ambao utapigwa leo saa 1 usiku
Shauku kubwa mashabiki wa Yanga leo ni kuona ni mchezaji gani ambaye atafungua kalamu ya magoli ya Yanga kwenye ligi msimu huu
Nzengeli alifunga bao la kwanza la msimu uliopita huku Mzize akifunga bao la pili na 83 katika msimu huo ambao Yanga ilitetea taji la ligi kuu kwa mara ya nne mfululizo
Ni bahati mbaya kwa Mzize ambaye leo huenda asiwe sehemu ya kikosi baada ya kupata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Wiliete uliopigwa Angola wiki iliyopita
Nyota wengine wote wako tayari kwa mchezo huo ambao utatoa taswira ya matarajio ya Wananchi msimu huu