Pacome apania makubwa zaidi msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Sep 2025
Pacome apania makubwa zaidi msimu huu

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua mwishoni mwa wiki iliyopita alikuwa sehemu ya kikosi kilichoichapa Wiliete Banguela ya Angola mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Pacome ametoa kauli ya kibabe kwa timu pinzani zitakazokutana na wababe hao wa Tanzania katika michuano yote.

Nyota huyo aliyeifunga Simba kwa mara ya tatu katika mashindano tofauti, alisema kwa kikosi kilichopo Jangwani anaamini kina uwezo wa kubeba ubingwa wa michuano yoyote wakikaza buti.

Pacome anayeitumikia Yanga kwa msimu wa tatu sasa, akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast, amekuwa na rekodi nzuri ya kufunga mabao 19 na asisti 14 katika misimu miwili iliyopita ya Ligi Kuu.

“Hata kocha tuliyenaye ni mzuri, anayetaka soka la ushindi kushambulia hasa wakati tunapokuwa na mpira, bila kusahau nidhamu wakati hatuna mpira,” alisema Pacome aliyekuwa akitajwa kama Mchezaji Bora wa Mwaka, japo tuzo hizo za msimu uliopita ziliota mbawa kimya kimya.

“Ni ngumu kukosa mataji msimu huu kutokana na ubora tulionao, licha ya kwamba wapinzani wetu nao wamejipanga vilivyo, lakini bado tunajiamini kwamba tuna uwezo wa kubadilisha mchezo wakati wowote.”

Kwa upande wake, Pacome msimu huu amepania kuendeleza makali yake na kufanya vyema zaidi ya misimu iliyopita

“Licha ya kuanza vyema kwa kuifunga Simba lakini hainifanyi kujiona bora, bado napambana kuhakikisha malengo ya timu yanatimia. Naamini Mungu atasaidia utakuwa msimu mzuri kwa timu na kwangu pia, kwa sababu tumeanza vyema ili tusimuangushe kocha kwa kufanya anayotuelekeza,” alisema

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’