Yanga kujaribu wapya michuano ya SportPesa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 May 2018
Yanga kujaribu wapya michuano ya SportPesa
Michuano ya SportPesa Super Cup itaanza Juni 03 mpaka Juni 10 katika uwanja wa Kasarani Nairobi, Kenya.

Yanga ni miongoni mwa timu zitakazoshiriki kutoka Tanzania pamoja na Simba, Singida United na JKU.

Yanga imeleta wachezaji watatu wa Kimataifa ambao wanajaribiwa ili waweze kusajiliwa kwa ajili ya michuano ya kombe la Shirikisho na msimu ujao.

Wachezaji wawili wametoka Jamhuri ya Kidemokrasi na Congo ambao ni kiungo Cedrick Kabale na mshambuliaji Alain Mulumba.

Yanga pia imemleta mshambuliaji kutoka nchini Nigeria Ugochukwu James ambaye pia yuko kwenye majaribio.

Wachezaji hao huenda wakatumiwa kwenye michuano ya Sportpesa nchini Kenya ili waweze kuonekana na pengine kusajiliwa kama viwango vyao vitamridhisha kocha Mwinyi Zahera.

Yanga inasaka mbadala wa Donald Ngoma baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa Mzimbabwe huyo.

Pia Yanga inahitaji kujaza nafasi ya Fiston Kayembe Kanku aliyesajiliwa lakini baadae ikabainika ana mkataba na timu nyingine licha ya jina lake kuwasilishwa CAF.

Taarifa za uhakika ni kwamba Yanga imevunja mkataba wake na sasa inakusudia kusajili mchezaji mwingine wa Kimataifa.

Kama CAF itaridhia kuondolewa kwa majina ya Donald Ngoma na Kayembe huenda Yanga ikaweza kuongeza hadi wachezaji watano kwenye kikosi chake kinachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’