Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amesema licha changamoto ya ratiba, kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Wiliete Sc ambao utapigwa kesho Ijumaa katika uwanja wa Novemba 11 nchini Angola
Yanga ilitua Angola jana katika mji wa Luanda ambao mchezo huo utapigwa ambapo kikosi kitakuwa na siku moja tu ya kufanya mazoezi leo
Akizungumza katika mkutano na wanahabari, Folz alisema ratiba ni changamoto lakini sio kisingizio kwa sababu ana kikosi kipana ambacho atakitumia kwa kuzingatia ratiba hiyo
"Ni kweli tuna ratiba ngumu lakini sio sababu kwa kuwa tunapaswa kujiandaa kwa kuzingatia ratiba hiyo ambayo tutakabiliana nayo msimu mzima"
"Tuna kikosi kipana, wachezaji wote wako tayari na tutawatumia kwa kuzingatia mahitaji ya mechi husika," alisema Folz
Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Folz alisema wamejiandaa vyema, malengo ni kusaka ushindi licha ya kukiri anakutana na timu ambayo haifahamu vyema
"Mkakati wetu kuelekea mchezo huu hautabadilika, iwe unacheza nyumbani au ugenini katika michuano hii ya CAFCL, malengo makuu ni kupata matokeo mazuri na kujiwekea mazingira ya kusonga mbele hatua inayofuata"