Ligi kuu ya Vodacom inamalizika rasmi Jumatatu ijayo May 28 kwa timu zote nane kuteremka dimbani lakini leo May 23 kuna mchezo mmoja wa kiporo kati ya Ndanda FC dhidi ya Mwadui FC.
Michezo ya kiporo itakamilika keshokutwa Ijumaa May 25 kwa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting.
Mchezo wa leo una umuhimu wa kipekee kwa Ndanda FC kwani utabainisha hatma yao ya kubaki ligi kuu msimu ujao.
Ndanda yenye alama 23 iko nafasi ya pili kutoka chini juu ya Njombe Mji yenye alama 22.
Lakini juu ya Ndanda iko Majimaji FC yenye alama 24.

Kama Ndanda itaifunga Mwadui FC leo katika dimba lake la nyumbani, basi itakuwa katika nafasi nzuri ya kubaki ligi kuu msimu ujao kwani itafikisha alama 26.
Ushindi huo pia utakuwa umeishusha rasmi daraja Njombe Mji.
Kama haitaibuka na ushindi timu zote tatu zitakuwa na nafasi ya kujinusuru kwenye michezo yao ya mwisho itakayopigwa katika viwanja vyao vya nyumbani.
Timu mbili za chini ya msimamo ndizo zitateremka daraja.
May 28, Ndanda itacheza na Stand United, Njombe Mji na Mwadui FC wakati Majimaji watawakaribisha mabingwa wa msimu huu Simba.

ADVERTISE HERE