Folz ataingiaje kuikabili Simba leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Sep 2025
Folz ataingiaje kuikabili Simba leo?

Mashabiki wa Yanga SC wanasubiri kwa hamu kubwa kuona timu yao leo Jumanne, Septemba 16, 2025, itaanza vipi pambano la Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mechi hii si tu ni dabi ya Kariakoo, bali pia ni mtihani wa kwanza kwa kocha mpya wa Yanga, Romain Folz, kuonyesha mkakati wake na jinsi atakavyoendeleza ubabe wa Yanga mbele ya Simba.

Changamoto kubwa kwa Folz ni kuchagua wanaume 11 ambao watakuwa kiini cha ushindi wa Yanga leo. Mashabiki wanahitaji ushindi mwingine ili kulinda heshima na kuendeleza ubabe mbele ya Simba.

Kikosi cha Yanga sasa kimejaa wachezaji wenye vipaji vikubwa katika kila eneo, jambo linalompa Folz nafasi za kubadilisha na kurekebisha mkakati bila kuathiri ubora wa timu.

Eneo pekee ambalo kwa sasa linaonekana kushikiliwa vizuri ni mlinda lango, ambapo Djigui Diarra anaonekana kujiweka kama nguzo ya timu. Sehemu nyingine hazina mshindani mmoja tu, Folz ana wachezaji angalau wawili au zaidi kwa kila nafasi, jambo linalompa wigo mpana wa kuchagua.

Ikiwa Folz ataamua kuanza na kikosi kilichomaliza msimu uliopita kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Simba, Ataongeza mchezaji mmoja katika safu ya kiungo mkabaji, kuchukua nafasi ya Khalid Aucho aliyejiunga na Singida Black Stars.

Hapa ndipo mabadiliko yanaweza kuhitajika, Moussa Balla Conte au hata Aziz Andabwile, wanaweza kutumika vyema katika eneo hilo

Folz pia anaweza kufanya mabadiliko katika safu ya ulinzi. Wachezaji kama Mohammed Hussein, Frank Assink, na Bakari Mwamnyeto wanaweza kutumika pia.

Eneo la mbele lina wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa; Mohamed Doumbia, Lassine Kouma, Celestin Ecua, Offen Chikola na Andy Boyeli wote wako tayari kuikabili Simba leo.

Ni wazi Yanga inakwenda katika mchezo huu ikiwa na kikosi bora zaidi. Mashabiki wanaweza kutarajia mechi yenye ushindani mkali, mikakati ya kitaalamu na matarajio ya wachezaji wao kuonyesha ubora wao mbele ya watani wa jadi.

Kwa maneno mengine, Folz ana kila silaha muhimu ya kuikabili Simba, mchezo wa leo unaweza kuwa mwanzo wa enzi mpya ya Yanga chini ya kocha huyo raia wa Ufaransa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’