Baada ya kukabidhiwa hati, ujenzi wa uwanjani ni suala la muda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Sep 2025
Baada ya kukabidhiwa hati, ujenzi wa uwanjani ni suala la muda

Siku chache zilizopita historia mpya iliandikwa kwa Wananchi wa Yanga SC. Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, klabu hiyo kubwa nchini ilikabidhiwa rasmi hati ya eneo la Jangwani litakalotumika kwa ujenzi wa uwanja wake wa kisasa.

Tukio hilo lililofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, limefungua ukurasa mpya wa maendeleo ndani ya klabu na kuongeza matumaini kwa mashabiki kwamba ndoto ya kumiliki uwanja wa kisasa inakaribia kuwa halisi.

Juzi, Kamati ya Utendaji ya Yanga ilikutana Makao Makuu ya klabu, Jangwani, kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya klabu. Kikao hicho kilifanyika siku moja tu baada ya kukabidhiwa hati ya eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 37,500, hatua muhimu kuelekea ujenzi wa uwanja huo

Mdhamini na mfadhili wa klabu, Ghalib Said Mohammed (GSM), ameridhia rasmi ombi la Wananchi kujenga uwanja huo, ambao unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 20,000.

Ni mradi mkubwa wenye thamani ya kihistoria, kwani kwa mara ya kwanza mashabiki wa Yanga watakuwa na makao yao ya kudumu katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, amewahakikishia wanachama na mashabiki kwamba ujenzi wa uwanja wa Jangwani ni kipaumbele chake namba moja. Ameahidi kwamba kabla ya kumaliza muda wake wa uongozi, atahakikisha ndoto hiyo inatimia

Uwanja wa Jangwani si tu eneo la kuchezea mpira. Ni alama ya heshima, urithi wa vizazi, na kielelezo cha hadhi ya klabu yenye historia kubwa ya soka Tanzania Bara na Afrika. Wananchi wanatarajia kuona si tu uwanja wa mechi, bali pia kituo cha biashara, burudani na maendeleo ya kijamii kitakachoinua hadhi ya Yanga ndani na nje ya uwanja.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’