Baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba hapo kesho, kikosi cha Yanga kitaondoka nchini kuelekea Angola tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Wiliete Banguela
Ratiba inaonyesha mchezo huo utapigwa Septemba 19 katika uwanja wa Novemba 11 huko Angola, saa 12 jioniΒ
Hivyo baada ya mtanange dhidi ya Simba, Wananchi watakuwa na siku tatu kuelekea mchezo dhidi ya Wiliete. Hapa ndipo umuhimu wa kuwa na kikosi kipana utaonekana
Wakati akiongea katika mkutano na wanahabari siku tatu zilizopita kuelekea mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Bandari Fc, mkufunzi wa Yanga Romain Folz aliweka bayana kuwa ameiandaa timu yake kukabiliana na ratiba ya mechi zinazofuatana karibu karibu ambayo itawakabili msimu huu
Wakitoka Angola, Yanga wanakabiliwa na mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji utakaopigwa Septemba 24 kisha kurudiana na Wiliete siku tatu baadae
Β