Klabu ya Al Ahly Tripoli ya Libya imeonesha dhamira ya dhati ya kumsajili mshambuliaji matata wa Young Africans, Clement Mzize, lakini bado imegonga mwamba.
Ujumbe wa viongozi wakubwa wa klabu hiyo, ukiongozwa na Rais Mohamed Al-Mashai na tajiri wa klabu, Prof. Ismail Al-Shtiwi, ulifika Tanzania kwa mazungumzo ya ana kwa ana na uongozi wa Yanga. Lengo kuu lilikuwa ni kushawishi mabingwa hao wa Tanzania Bara kuachia nyota wao.
Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza wazi kuwa uongozi umeendelea kusimama kidete kutomuuza Mzize, kwa kigezo cha kutanguliza malengo ya kimataifa msimu huu.
Yanga imepanga kufanya vyema zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na michuano mingine ya CAF, jambo linalowafanya washindwe kuzingatia dau lolote kwa sasa.
Ili kuongeza hamasa na kumfanya aendelee kubaki klabuni, tayari Yanga imefanya maboresho makubwa kwenye mshahara na marupurupu ya bonasi kwa Mzize.
Hatua hiyo inalenga kumjengea motisha mpya kuelekea msimu ujao wa mashindano yote, huku ikitarajiwa kwamba atakuwa nguzo muhimu ya safu ya ushambuliaji ya Wananchi.
Mzize bado ana mkataba wa miaka miwili na Yanga, ambapo kwa mujibu wa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema ataendelea kutumikia mkataba huo