FT : Yanga 1-0 Bandari Fc, kilele wiki ya Wananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Sep 2025
FT : Yanga 1-0 Bandari Fc, kilele wiki ya Wananchi

Yanga imehitimisha shamrashamra za wiki ya Wananchi kibabe wakiichapa Bandari Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Siku iliyosheheni kila aina ya burudani ikafika tamati kwa mchezo huo ambao ulishuhudia kiungo mshambuliaji Celestin Equa akifunga bao pekee la ushindi katika dakika ya 3 akimalizia krosi ya Prince Dube

Ulikuwa mchezo wa vipindi viwili tofauti mkufunzi wa Yanga Romain Folz akitumia vikosi viwili tofauti katika kila kipindi

Yanga ilitawala na kucheza kwa kasi kubwa pengine ilistahili kupata ushindi mnono kwa kuzingatia nafasi walizopoteza hasa katika kipindi cha kwanza

Unaweza kusema Wananchi leo wameonjeshwa radha ya kile watakachokishuhudia msimu huu, pengine chakula kamili watakipata katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Septemba 12

Folz leo alipumzisha baadhi ya nyota wake muhimu kama Pacome Zouzoua na Clement Mzize ambao hawakutumika kabisa wakati nyota wengine wapya Equa, Kouma, Assink, Moussa Balla Conte, Mohammed Doumbia, Chikola, Boyeli wakipata dakika za kuonyesha kile walichonacho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’