Wakati akizungumza na wanahabari jana, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alidokeza kuwa leo kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi, mashabiki watarajie kuwaona nyota wao wote muhimu wakishuka dimbani
Kumekuwa na changamoto ya ratiba ambapo ni takribani siku nne tu zimebaki kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa Septemba 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kamwe alisema Yanga ina kikosi imara na hivyo hawatakuwa tayari kuwanyima burudani mashabiki wao kwa kuhofia mchezo unaofuata dhidi ya Simba
"Niwahakikishie mtaiona Yanga ileile sisi hatuogopi mtu, tutashusha kikosi chetu kamili na tutacheza katika daraja letu na uchu uleule ili tukate kiu ya burudani kwa mashabiki wetu"
"Haiwezekani kila siku tunawasifia akina Mohamed Doumbia halafu mashabiki waje uwanjani wasiwaone kweli?," alitamba Kamwe
Kauli hiyo ilipigiliwa msumari na kocha mkuu wa Yanga Romain Folz ambaye alisema mchezo dhidi ya Bandari Fc leo hauwezi kuwaathiri kwa sababu wamejiandaa kucheza mechi katika muda mfupi
"Ukiangalia ratiba, kuna mechi nyingi tutacheza kila baada ya siku tatu, nne na ukiangalia baada ya mchezo dhidi ya Bandari Fc, tutakuwa na siku nne kuelekea mchezo dhidi ya Simba"
"Nafikiri haiwezi kuwa changamoto kwa sababu katika msimu huu tumejiandaa kucheza katika utaratibu huo wa ratiba, "alisema Folz
Hivyo Bandari Fc watarajie kushushiwa 'Busta' zote za Wananchi pengine katika dakika 20 za kwanza na kisha Folz kubadili kikosi chake ili kumpa nafas kila mchezaji katika siku hii ya furaha kwa Wananchi