Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amesema kikosi chake kiko tayari kushuka uwanjani kesho Ijumaa katika kilele cha wiki ya Mwananchi uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Folz alisema wamewaandalia mashabiki burudani kubwa katika mchezo huoa ambao anauchukulia kama sehemu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea msimu mpya
"Tumejiandaa vyema kwa tukio kubwa hapo kesho, tunausubiri mchezo huo kwa shauku kubwa. Utakuwa mchezo wetu wa mwisho katika maandalizi yetu ya pre-season, tutahakikisha tunawapa burudani mashabiki wetu wakaokuja kwa wingi kutuunga mkono"
"Sisi tunachukulia kila mchezo kwa uzito mkubwa, hatutakuwa na mechi ndogo au kubwa dhumuni hapa ni kuhakikisha tunafnya vyema katika kila mchezo. Pengine tofauti pekee ya mchezo wa kesho ni siku ya Yanga, tutakuwa na sapoti kubwa ya mashabiki wetu uwanjani hili linaweza kuwaongeza wachezaji morali"
"Lakini kiufundi naweza kusema hakuna kitu kitabadilika vile tutaukabili mchezo huo ni vilevile tutakavyokabili mechi nyingine," alisema Folz
Folz amesema ana kikosi chake kamili baada ya wachezaji wote waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa kurejea
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto amesema wachezaji wote wako tayari kuwapa burudani mashabiki wao hapo kesho
"Tumekuwa na wakati mzuri wa maandalizi, tumecheza mechi kadhaa za kirafiki ambazo zimewasaidia walimu kufanya maboresho zaidi na kuhakikisha tuko imara"
"Nawaomba Wananchi wajitokeze kwa wingi uwanjani waje kuona kile tulichowaandalia," alisema