Leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani ilifanyika dua maalum kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/26
Dua iliwakutanisha mashabiki na wanachama wa Yanga kutoka kila pembe ya nchi kuiombea timu yao ipate kuwa na msimu mzuri
Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji aliungana na Wananchi katika dua hiyo ambapo alitoa salamu za shukrani kwa wote waliojitokeza
Arafat amesema ni kawaida kwa wanayanga kumuomba Mungu, huu ni kwa sababu Yanga inaamini sana katika ibada
"Tunawashukuru viongozi wote wa kiroho waliofika Jangwani leo kwa ajili ya dua. Viongozi wengi wametoka mbali ikiwemo mchungaji aliyetokea Mwanza"
"Ni wazi kuwa klabu hii inagusa sana hisia za walio wengi. Kumuomba Mungu kabla ya msimu kuanza imekuwa jadi yetu kwani tunaamini sana katika ibada"
"Msisite kuendelea kutuombea. Mtuombee afya njema, amani na Mungu atuepushe na kila shari, husda mikosi na balaa,” alisema Arafat



