Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amefichua kuwa kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi siku ya Ijumaa pale uwanja wa Benjamin Mkapa atakuwa sehemu ya washereheshaji (MC)
Katika misimu ya karibuni Yanga imewatumia Dacota, Zembwela na Maulid Kitenge kama washereheshaji wakuu huku Haji Manara akiingia kwenye utambulisho wa wachezaji
Ni wazi siku ya Ijumaa huenda Kamwe akaungana na timu hiyo hasa katika eneo la utambulisho wa kikosi
"Kwenye siku ya Mwananchi hamjawahi kuniona katika kipaza au eneo lolote nikifanya vurugu zangu. Niwaambie tu, mwaka huu nimo"
"Mimi ni kisima cha burudani na wote mnajua, nikishaingia hakuna binadamu yoyote atakayejadili mtu mwingine zaidi yangu, nitaishtua dunia," alitamba Kamwe
Kamwe anatarajiwa kuleta radha tofauti kwenye utambulisho wa kikosi