Yanga inaendeleza ubabe pre-season licha ya kuwakosa mastaa 11

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Sep 2025
Yanga inaendeleza ubabe pre-season licha ya kuwakosa mastaa 11

Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz anaendelea kukiandaa kikosi chake kuelekea Yanga Day, Septemba 12 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Jana Yanga ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya JKT Tanzania na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, mchezo uliopigwa dimba la Isamuhyo

Licha ya kuwakosa wachezaji 11 ambao wako katika majukumu ya timu za Taifa, Yanga imeendeleza rekodi ya ushindi katika mechi za kirafiki

Huo ulikuwa mchezo wa nne Yanga inashinda baada ya pia kuzifunga Rayon Sports (3-1), Fountain Gate (2-1) na Tabora United (4-0)

Wachezaji walioitwa katika timu za taifa ni kipa Diarra Djigui (Mali), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya, Edmund John na Clement Mzize waliopo katika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ambayo usiku wa jana walikuwa ugenini dhidi Congo Brazzaville katika mchezo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Wengine ni, Lassine Kouma na Celestin Ecua waliopo Chad, Balla Moussa Conte katika kikosi cha Guinea na Duke Abuya timu ya Taifa ya Kenya

Moja ya sababu iliyopelekea Yanga kupelekea kilele cha wiki ya Mwananchi Septemba 12 ni pamoja na kuzingatia kalenda ya FIFA ambapo mechi za kuwania kufuzu kombe la Dunia zitamalizika Septemba 09

Nyota walio katika majukumu ya timu za Taifa watakuwa na muda wa kuwahi Tamasha hilo la Wananchi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’