Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amefanikisha ujio wa wachezaji wawili, kiungo Cedrick Kabale na Alain Mulumba watakaojaribiwa kabla ya kusajiliwa.
Wachezaji hao wawili wametoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kama watafuzu majaribio yao huenda wakaongezwa kwenye kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mulumba mwenye umri wa miaka 29, anatokea klabu ya DC Motema Pembe ya Ligi Kuu ya DRC, ana uwezo wa kucheza nafasi zote za wingi na mshambuliaji wa kati.
Kabale ambaye ndio kwanza ana miaka 21 anatokea klabu ya Don Bosco ya Ligi Kuu DRC.
Yeye ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mchezeshaji na mshambuliaji wa pili.
Yanga pia inamjaribu mshambuliaji kutoka Nigeria, Ugochukwu James ambaye huenda akachukua nafasi ya Donald Ngoma anayedaiwa kuondolewa kikosini na kocha Zahera.
Aidha habari zaidi zinabainisha kuwa Zahera amepania kumleta mlinda lango wa timu ya Taifa ya DRC Vumi Ley Matampi aliyedaka kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzania March 27.
Kipa huyo ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba kwenye klabu ya TP Mazembe.

ADVERTISE HERE