Tetesi zinazodai kuwa Yanga inafikiria kumrudisha kiungo Khalid Aucho hazina ukweli wowote kwani tayari Wananchi wamefunga usajili wa nyota wa kigeni
Yanga imekamilisha idadi ya wachezaji 12 wa kigeni ambao ni Djigui Diarra, Frank Assink, Moussa Balla Conte, Maxi Nzengeli, Celestine Ecua, Lassine Kouma na Prince Dube
Wengine ni Andy Boyeli, Pacome Zouzoua, Duke Abuya, Chadrack Boka na Mohamed Doumbia
Aucho anatajwa kujiunga na klabu ya Singida Black Stars akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika
Yanga ilimpa tuzo ya heshima Aucho baada ya utumishi wake wa miaka minne akiwa na Wananchi
Conte ndiye anayetarajiwa kuchukua nafasi yake huku pia Yanga ikiwa na uhakika wa kuwatumia katika nafasi hiyo nyota wengine kama Duke Abuya, Mudathir Yahya na Salum Aboubakar
Lakini pia kinda Abdulnasir Abdallah 'Casemiro' anaweza kutumika pia katika eneo hilo la kiungo cha ukabaji