Tutaanza na Ngao ya Jamii - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Aug 2025
Tutaanza na Ngao ya Jamii - Arafat

Klabu ya Yanga imeanza mikakati kabambe ya kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao wa jadi, Simba, unaotarajiwa kupigwa, Septemba 16, mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Makamu wa Rais, Arafat Haji, amesema juzi kuwa mipango na mikakati ya mechi hiyo imeshaanza ambapo lengo ni kupata ushindi ili kuendelea kulihifadhi taji hilo.

Arafat amesema kuwa heshima ya Yanga kwa msimu wa 2025/26, itaanza kuwekwa katika mchezo huo.

"Tuna kazi tarehe 16, jamaa walitamani ule mfumo ungeendelea, walitamani ungendelea kuchezwa kwa mfumo wa nusu fainali ili watukimbie tena, lakini wanasema Mungu si Athumani, kawaleta, siku hiyo tutaanza kuweka heshima ya Yanga kwa msimu wa 2025/26,” alisema Haji. Akaongeza:

“Tutakwenda kuhakikisha Ngao ya Jamii inakwenda nyumbani, ibakie Jangwani kwa sababu ni kwao, hivyo ushirikiano wa Wanayanga wote ule uliooneshwa msimu uliopita uongezeke mara dufu msimu huu."

Hivi karibuni, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), lilitangaza mabadiliko ya Kanuni ya Ligi Kuu msimu huu ambapo badala ya kucheza mechi tatu, nusu fainali mbili na fainali moja, kwa timu nne kushiriki, badala yake itacheza mechi moja tu.

Kwa mujibu wa TFF, mchezo huo utahusu bingwa wa Tanzania Bara ambaye ni Yanga, watakaocheza na mshindi wa pili wa Ligi Kuu, Simba. Imesema timu hizo zitalazimika kucheza mechi hiyo kutokana na kanuni.

Yanga ilibidi icheze na bingwa wa Kombe la FA, lakini kwa sababu yenyewe ndiye bingwa pia wa makombe yote mawili, hivyo kanuni inasema itacheza na mshindi wa pili wa Ligi Kuu.

TFF, ilifafanua kuwa mfumo wa mashindano hayo umebadilika msimu huu kutokana na marekebisho ya kanuni zilizopitishwa hivi karubuni na Kamati ya Utendaji ya TFF.

Moja ya marekebisho hayo yanasema ikitokea mazingira kama ya sasa ambapo mashindano yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) yamebana ratiba za TFF itachezwa mechi moja tu ya Ngao ya Jamii.

Kwa sasa Tanzania ni mwenyeji wa fainali za CHAN zilizoanza Agosti 2 mwaka huu, zitakazomalizika Agosti 30. Kwa mfumo wa kawaida, Yanga ilitakiwa kucheza dhidi ya Azam FC, katika mchezo wa nusu fainali, huku Simba ikitakiwa kucheza dhidi ya Singida Black Stars.

Yanga imeifunga Simba mara tano mfululizo, mara nne kwenye mechi za Ligi Kuu kwa misimu miwili mfululizo, nyumbani na ugenini pamoja na mchezo mmoja wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii uliochezwa, Agosti 8, mwaka jana.

Msimu uliopita, Yanga ilitwaa Ngao ya Jamii kwa kuichakaza Azam, mabao 4-1 yaliyofungwa na Prince Dube, Yoro Diaby aliyejifunga mwenyewe, Stephane Aziz Ki na Clement Mzize, huku bao la Azam ambao walitangulia likifungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ Agosti 11, mwaka jana, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’