Zahera kuiendesha Yanga kidigitali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
22 May 2018
Zahera kuiendesha Yanga kidigitali
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameahidi kurejea na vifaa maalum vitakavyomsaidia kupima maendelea ya wachezaji wake.

Zahera alirejea DR Congo kwa majukumu ya timu ya Taifa ambapo May 28 ataiongoza timu hiyo kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria.

Vifaa hivyo vyenye GPS vina uwezo wa kupima kasi na uwezo wa mchezaji katika kuhimili mikikimikiki kwa muda mrefu.

Katika mahojiano na gazeti la Mwanaspoti, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika amesema Zahera ameahidi kununua vifaa hivyo kwa pesa zake na atakuja navyo wiki ijayo baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa.

Nyika amesema Zahera amepania kubadilisha mambo mengi katika kikosi na anataka kujua kila mchezaji ana uwezo gani wa kukimbia na anataka kuona uwezo wa mwili wake kuwa tayari kwa mazoezi hayo na kuamua kuleta vifaa hivyo.

Amesema mara baada ya kuleta vifaa hivyo atavitumia kuangalia ubora wa wachezaji hao na watakaoonekana na uwezo mdogo wataondolewa haraka huku watakaosalia wataanza mazoezi makali ya kocha huyo.

Zoezi la kuwapima mara kwa mara litaendelea na kama watabainika wengine kushuka uwezo wanaweza kuondolewa.

“Kocha anaonyesha yuko siriazi kweli na kazi yake tulikutana naye kama kamati na akatuambia anaenda kwao, kule kuna vifaa maalumu atakavyorudi navyo, ili kutumia kuwapima wachezaji,” alisema Nyika.

“Vifaa hivyo ni maalumu kupima uwezo wa mchezaji kukimbia, pia uwezo wa mwili wake kuweza kuhimili mazoezi ambayo atakuwa anayatoa, kilichotushangaza tulitaka tumsaidie kununua lakini ametuzuia amesema atakuja navyo mwenyewe.”
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →