Chyna awakimbiza nyota Yanga mchangani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2025
Chyna awakimbiza nyota Yanga mchangani

Mtaalam wa mazoezi ya viungo Chyna Mokaila leo aliwapeleka wachezaji wa Yanga ufukweni ikiwa ni program maalum ya mazoezi ya kujenga utimamu wa mwili

Akiwa katika wiki ya pili ya pre-season, Chyna ameendelea kuwajengea wachezaji 'fitness' na pumza tayari kwa mikiki mikiki ya msimu ujao wa mashindano 2025/26

Chyna amesema mazoezi ya ufukweni ni maalum kuimarisha utimamu wa miili ya wachezaji wake na kuwaweka tayari kucheza dakika 90 au zaidi na pia kuwaepusha na majeraha

"Lengo kuu la mazoezi haya ni kuimarisha fitness ya wachezaji wetu, unajua wametoka kwenye mapumziko 'off-season' sasa lazima tuitoe miili yao katika hali ya mapumziko na kuwaweka tayari kucheza dakika 90 au zaidi pasipo kupata majeraha"

"Nina kawaida ya kuwapeleka gym nyakati kama hizi lakini leo nimechagua kuwapa mazingira tofauti ili kuona kwa kiasi gani wanaweza kuhimili mazoezi ya mchangani"

"Yanga ni timu kubwa hivyo ni lazima kila mmoja ajitoe kwa asilimia 100, nafurahi kufanya kazi na kundi hili la wachezaji ambao wanajituma na kutimiza vyema majukumu yao," alisema Chyna

Yanga ilirejea mazoezini jana baada ya mchezo dhidi ya Rayon Sports Ijumaa iliyopita ambao Yanga ilishinda kwa mabao 3-1 na kutwaa taji la Rayon Day huko Rwanda

Kumekuwa na angalau 'session' mbili za mazoezi kwa siku ambapo asubuhi yanafanyika mazoezi kuimarisha utimamu wa mwili na jioni mazoezi ya mbinu uwanjani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’