Mabadiliko Yanga hayaepukiki - Tarimba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
21 May 2018
Mabadiliko Yanga hayaepukiki - Tarimba
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Abbas Tarimba amesema kuwa mabadiliko Yanga yalianza siku nyingi, zama za aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo, George Mpondela ‘Castro’ (marehemu), ambaye hata hivyo alipingwa mawazo yake.

Lakini amesema mchakato huo sasa hauepukiki kwa klabu ya Yanga.

Katika mahojiano yake hivi karibuni, Tarimba alisema mabadiliko Yanga hayawezi kuepukika, isipokuwa suala la msingi ni kuangalia ni ya aina gani ya mabadiliko yanayotakiwa kwa sasa kwa klabu hiyo kubwa nchini.

“Safari ya mabadiliko Yanga ilianza zamani, siku nyingi mabadiliko yametakiwa, lakini lazima tujiulize, ni ipi haja ya mabadiliko haya ya sasa,” alieleza Tarimba.

Tarimba, ambaye hata hivyo hakutaka kuingia kwa undani kwenye suala hilo la mabadiliko Yanga, alieleza uendeshaji wa klabu hiyo na nyinginezo kwa sasa lazima ubadilike, hata kama siyo wa kutumia mfumo kama ambao umekuwa ukipendekezwa.

Amesema mchakato huo wa mabadiliko Yanga hauepukiki kwa nyakati hizi.

Tarimba amesema Yanga imechelewa kuingia katika uendeshaji mpya ambao ulianzishwa miaka ya 1990, lakini haukuwapendeza baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa.

“Hili wazo la mabadiliko alikuja nalo Mpondela, halijaanza leo wala jana, lilikuwepo tangu miaka ya ‘90, lakini wafadhili wa Yanga wa wakati ule hawakulifurahia,” alisema.

“Haja ya kubadilika ipo na hili suala nasema haliepukiki, lakini tunabadilikaje, ndiyo suala la msingi kujadiliwa, wanachama waelezwe faida na hasara za mabadiliko hayo kabla ya kuridhia mwenendo mpya wa uendeshaji wa klabu,” alisisitiza.

Akizungumzia mpango wa mabadiliko na kuifanya Yanga kuwa kampuni enzi za uongozi wake na kuigawa klabu vipande, Tarimba alisema ulitokana na baadhi ya wanachama kuwa wapinzani ndani ya klabu.

“Kuna wanachama huwa ni wapinzani tu, kazi yao wao ni kupinga kile ambacho kinafanywa na uongozi, wakati nikiwa mwenyekiti waliibuka, tulipokuja na wazo la kuiendesha Yanga kama kampuni walitupinga.

“Ilitokea baadhi yetu wakajitenga na kujiita Yanga Asili, hao hawakupenda mfumo ule wa mabadiliko, nakumbuka ilileta mgogoro mkubwa, wenzetu wao walikuwa wakikutana maeneo ya Keko, tulipaita kwenye machuma.

“Mgogoro huo ulikuwa mkubwa. lakini kwa masilahi ya klabu tulitafuta mwafaka na mambo yakawa vizuri, hata sasa, mabadiliko ni lazima, lakini yafanywe kwa uwazi na wanachama waanze kwa kuelimishwa na kuambiwa nini faida na zipi hasara,” alisema Tarimba,

Serikali kupitia Baraza la Taifa la Michezo (BMT) tayari imetoa mwongozo wa kufuata kwa vilabu vinavyofanya mabadiliko ya uendeshaji wake.

Simba imekuwa klabu ya kwanza kufanya mabadiliko ambapo jana ilifanya marekebisho ya katiba yake na kuruhusu uwekezaji wa Bilionea Mohammed Dewji ambaye atanunua hisa asilimia 49 za klabu huku asilimia 51 zikibaki kwa Wanachana kupitia Kampuni yao watayounda.

Muundo huu pia ndio unaopendekezwa kwa klabu ya Yanga ambayo tayari imeitisha Mkutano Mkuu Juni 17 2018 kufanya mabadiliko ya Katiba yake ili iendane na mwongozo wa Serikali.

Pia kwenye Mkutano huo Yanga itafanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi (nafasi ya Mwenyekiti).

Jina la Abass Tarimba, Mwenyekiti wa zamani wa Yanga ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuwania nafasi ya Mwenyekiti.

Mwenyewe ameunga mkono mawazo ya wanachama wanaomtaja kwa kusema wakati ukifika huenda akafikiria kuchukua fomu.

“Wana Yanga wakinitaja kuwemo katika wale wanaofikiria wanafaa kuwa viongozi wa klabu kwangu mimi ni heshima kubwa sana na niwashukuru wanayanga kwa kunifikiria hivyo.”

“Niseme nimelisikia na kuliona ni jambo muhimu sana ingawa tunaita ni fitina za kimichezo lakini mimi binafsi nalipa ukubwa sana na ninalifikiria vizuri kwa sababu na mimi ningependa Yanga ifanye vizuri na kama nina weza kutoa mchango kwa klabu yangu kwa nini nisifanye hivyo?

“Kwa kuwa wanayanga wanaona naweza kuchangia kwa namna moja ama nyingine nikiwa kiongozi wao si vibaya kulifikiria. Kama itatangazwa masuala ya uchaguzi nitafikiria sana hili,” amesema Tarimba
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →