Dozi yao maalum inaandaliwa - Kamwe atamba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2025
Dozi yao maalum inaandaliwa - Kamwe atamba

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa ushindi wa mabao 3-1 ambao wamepata juzi huko Rwanda na kutwaa taji la Rayon Day, ni ishara ya ubora wa kikosi chao

Kamwe amesema licha ya kufanya mazoezi kwa takribani siku 10, wameweza kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Rayon Sports, timu yenye historia kubwa Rwanda

"Niwaambie mashabiki na wanachama wa Yanga, walichokiona katika mchezo dhidi ya Rayon Sports kilitengenezwa kwa siku 10 tu. Haijawahi kutokea duniani timu ikawa na siku 10 kwenye pre-season halafu ikaonyesha kiwango cha aina ile"

"Kwa kawaida kwenye pre-season wiki za mwanzo unajenga fitnes ya wachezaji lakini angalia ubora tulioonyesha dhidi ya Rayon. Wachezaji ndio kwanza wamekutana na kila mmoja ameonyesha uwezo wake"

"Bado kocha ana kazi ya kutengeneza muunganiko, pale kila kitu kitakapokaa sawa itakuwa hatari. Mashabiki na Wanachama wa Yanga wala tusiongee sana, tuwe watulivu wakati mambo yanaendelea kupikwa lakini niwahakikishie hiki kikombe kuna mtu atakinywa," alitamba Kamwe

Katika hatua nyingine Kamwe ametamba sio kila timu inaweza kushinda mechi za pre-season kama inavyofanya Yanga

Kamwe amewapiga dongo watani zake Simba baada ya kufungwa mabao 4-3 na ENPPI hapo jana katika mchezo wa kirafiki huko Misri, maafisa wa timu hiyo wakificha matokeo ya mchezo huo ambao ulishuhudiwa na balozi wa Tanzania huko Misri

"Mficha uchi tayari kaanza kuagiza maembe," aliandika Kamwe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’