Ndio tumepoteza ubingwa, lakini kuendelea kufungwa hakuisaidii Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 May 2018
Ndio tumepoteza ubingwa, lakini kuendelea kufungwa hakuisaidii Yanga
Matokeo ya sare dhidi ya Singida United na baadae Mbeya City ndiyo iliyoiondoa rasmi Yanga kwenye mbio za ubingwa msimu huu.

Yanga iliutema rasmi ubingwa wa VPL siku ilipolazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City kwenye mchezo ambao ulijaa kila aina ya vituko.

Uwanja wa Sokoine uligeuzwa kuwa uwanja wa vita!

Kwenye mchezo huo tulishuhudia mashabiki wa Mbeya City wakiwapiga mawe wachezaji wa Yanga hasa mlinda lango Youthe Rostand aliyelazimika kulikimbia lango mara kadhaa ili kunusuru maisha yake.

Jeshi la Polisi lilitumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki wa Mbeya City waliokuwa wakirusha mawe uwanjani.

Wakati mchezo ukielekea ukingoni ikashuhudiwa tena Mbeya City wakicheza 11 uwanjani licha ya kuwa mchezaji mmoja alikuwa ametolewa nje kwa kadi nyekundu.

Baada ya michezo hiyo Yanga imeshindwa kurudi kwenye kiwango chake na kujikuta ikicheza sasa michezo tisa bila ya kupata ushindi.

Sawa, kuna wakati morali ya wachezaji ilishuka hasa baada ya kupoteza ubingwa ukichanganya na changamoto zinazowakabili klabuni.

Lakini kikosi hiki cha Yanga kinaenda kuandika historia 'mbaya' ya kucheza michezo mingi bila ya kushinda.

Thomas Kipese, mmoja wachezaji waliowahi kuitumikia Yanga, katika mahojiano yake na gazeti moja la kila siku anasema hana kumbukumbu ya kuwahi kuishuhudia Yanga ya aina hii.

"Sijawahi kuona hivi. Yanga siyo timu ya kutopata ushindi mechi nyingi mfululizo hivyo. Mimi nazijua Simba na Yanga. Simba imeshawahi kuwatokea mara nyingi, lakini Yanga ni timu ambayo ikifungwa leo, mechi ijayo itashinda, ikitoka sare mechi moja na nyingine ikifungwa inayofuata itashinda."

Lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti Yanga imefungwa michezo minne mfululizo ya ligi kuu ya Vodacom.

Yaani katika michezo tisa iliyopita, Yanga imefungwa michezo sita na kuambulia sare michezo mitatu pekee.

Yanga inalazimika kushinda michezo yake mitatu ya ligi iliyobaki ili kurejesha imani ya mashabiki wake.

Kuendelea kucheza mda mrefu bila kushinda kutashusha thamani ya klabu mara dufu na huenda ikawa na wakati mgumu sana kurejesha ule 'U-Yanga' wake.

Moja ya changamoto inayoikumba Yanga sasa ni kutokuogopwa na wapinzani wake.

Mwenendo huu mbovu umepelekea kila timu inayokumbana na Yanga kuamini inaweza kushinda. Timu hazina tena ile hofu ya kuwa zinacheza na Yanga.

kuhofiwa na mpinzani wako ndiyo silaha ya kwanza kuelekea kwenye ushindi.

Lakini kama mpinzani wako hakuhofii, lolote linaweza kutokea na hicho ndicho kinachoitesa Yanga sasa.

Ni lazima timu ianze kushinda ili irudishe heshima yake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’