Yanga kurejea mazoezini baada ya ushindi Rwanda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Aug 2025
Yanga kurejea mazoezini baada ya ushindi Rwanda

Baada ya kurejea kutoka Rwanda, Kikosi cha Yanga kitaendelea na maandalizi ya msimu mpya chini ya Kocha Mkuu Romain Folz, ambaye sasa ana takribani wiki tatu muhimu za kuhakikisha “Wananchi” wanakuwa tayari kwa changamoto za ndani na kimataifa.

Juzi, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rayon Sports kwenye uwanja wa Amahoro, mchezo uliokuwa sehemu ya Tamasha la Rayon Day. Licha ya kuwa mechi ya kirafiki, ilivutia hisia kubwa kutokana na ukubwa wa timu zote mbili na historia yao.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Folz alisisitiza kuwa ushindi pekee hauonyeshi sura kamili ya kikosi chake.

“Hii ni mechi ambayo imekuja wakati tuko mwanzo wa maandalizi yetu ya pre-season, nafurahi kuona wachezaji wangu wamepambana na kushinda, ingawa kiuhalisia bado hatufikia kile tunachotaka. Baada ya mchezo huu sasa tutakuwa na muda zaidi wa kufanya kazi kwenye uwanja wa mazoezi,” alisema kocha huyo raia wa Ufaransa.

Kwa mujibu wa Folz, kabla ya kukutana na Rayon, Yanga ilikuwa imefanya mazoezi kwa takribani siku 10 tu ambapo asilimia 75 ya mazoezi ilihusisha utimamu wa mwili, huku mazoezi ya mbinu yakipewa nafasi ya asilimia 25 pekee.

Baada ya kurejea kutoka Rwanda jana, kikosi cha Yanga kinaanza awamu ya pili ya maandalizi Jumatano hii kwenye uwanja wa KMC Complex ambapo nguvu kubwa itawekwa kwenye mbinu

Hii itakuwa nafasi kwa Folz kuimarisha mifumo ya uchezaji na kuzipa nafasi mbinu ambazo amekuwa akizihubiri tangu aingie klabuni. Kipimo kingine kwa timu yake kitafuata katika mchezo wa kilele cha Wiki ya Mwananchi kabla ya Ngao ya Jamii ambayo huenda wakakutana na Simba

Mashabiki wa Yanga wana sababu ya kujiamini. Kikosi kimeonyesha dalili njema kwa kipindi kifupi cha maandalizi, huku ushindi wa Kigali ukiwa kionjo cha kile kinachoweza kufanikishwa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’