Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa ufafanuzi kwa UMMA kuhusu mchango wa Shilingi Milioni 100 uliotolewa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) siku ya tarehe 12/08/2025
Taarifa iliyotolewa na Yanga mapema leo, imebainisha kuwa mchango huo ulitolewa na Taasisi y GSM Foundation iliyo chini ya Mdhamini na Mfadhili wa Yanga Ghalib Said Mohammed na sio kupitia hela za Wanachama au kutoka kwenye mfuko w klabu kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato
"GSM imekuwa ikishirikiana na klabu ya Yanga kwa kipindi cha miaka mitatu kutoa fedha na misaada kwa jamii na makundi mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya Tanzania"
"Uongozi wa Yanga unapenda kuomba radhi kwa Wanachama, Mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu kwa usumbufu wowote uliojitokeza kupitia sintofahamu hii, " ilibainisha taarifa ya Yanga
