Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alirejea DR Congo juzi kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa ambapo yeye ni kocha Msaidizi lakini atarudi nchini baada ya wiki moja.
Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano/Usajili ya klabu ya Yanga Hussein Nyika amesema baada ya kumalizana na kocha huyo kwa kumpa mkataba wa miaka miwili, sasa wanamsubiri arejee ili waanze kuisuka Yanga.
Nyika amesema usajili wa Yanga utafanyika kufuata mapendekezo ya kocha na si vinginevyo.
Kabla ya kusaini mkataba juzi, Zahera alipata muda wa kutosha kukifahamu kikosi cha Yanga na bila shaka mapendekezo yake yatakuwa na lengo kuondoa 'madhaifu' aliyoyabaini.
Dirisha la usajili linatarajiwa kufunguliwa mapema mwezi ujao na litafungwa mwanzoni mwa mwezi wa nane.

ADVERTISE HERE