Ijumaa ijayo August 15 Yanga itakuwa Rwanda kushiriki Tamasha la Rayon Sports Day, mabingwa hao wa Tanzania Bara wakialikwa na wenyeji wao
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewaalika Wanachama na Mashabiki katika safari ya kuelekea Rwanda
Yanga inatarajiwa kuondoka na msafara wa mashabiki kama walivyofanya misimu miwili iliyopita walipokwenda kucheza dhidi ya Al Merrikh mchezo wa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi CAF CL
Mechi dhidi ya Rayon itakuwa kipimo cha kwanza cha kikosi cha kocha Romain Folz kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/26 ambao Yanga imepania kuendeleza ubabe wake katika soka la ndani na kufanya nyema zaidi katika michuano ya ligi ya mabingwa
ADVERTISE HERE