Kiungo mshambuliaji Skudu Makudubela ambaye kwa sasa anaitumikia Wiliete Benguela ya Angola, atakabiliana na waajiri wake wa zamani Yanga katika mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa (CAF CL)
Yanga na Wiliete Benguela zitachuana mwishoni mwa Septemba mchezo wa kwanza ukitarajiwa kupigwa kati ya Septemba 19-21 huko Angola na marudiano kupigwa Septemba 26-28 jijini Dar es salaam
Skudu aliondoka Yanga msimu uliopita baada ya kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania kwa msimu mmoja akitokea klabu ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini

Wiliete Benguela walimaliza katika nafasi ya pili ligi kuu ya Angola msimu uliopita nyuma ya Petro Atletico waliotwaa ubingwa.
Skudu amejiunga na timu hiyo katika dirisha hili la usajili akitokea klabu ya AS Vita ya DR Congo ambayo alijiunga nayo mwezi Januari mwaka huu baada ya kukaa miezi sita bila ya timu