Klabu ya Yanga leo imesaini mkataba wa miaka mitatu wa udhamini kutoka kampuni ya Haier
Mkataba huo uliosainiwa hoteli ya Hyatt Dar es Salaam mbele ya Rais wa Yanga, Injini Hersi Said, una thamani ya Tsh Bilioni 3.3
Haier itakuwa moja ya wadhamini wa Yanga Sc kuelekea msimu ujao ambapo nafasi yao katika jezi mpya za mashindano zitakazozinduliwa hivi karibuni, itakuwa kwenye bega la mkono wa kushoto
Ifahamike Haier sio mdhamini mkuu, bali anaungana na Wadhamini wengine huku kampuni SportPesa ikiendelea kuwa Mdhamini Mkuu wa Yanga
ADVERTISE HERE