Mudathir amewatumia ujumbe viungo wapya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Aug 2025
Mudathir amewatumia ujumbe viungo wapya Yanga

Licha ya usajili mkubwa uliofanywa na Yanga katika dirisha hili, ni wazi nyota wapya watakuwa na kazi ya kufanya kujihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza

Ushindani unatarajiwa kuwa mkali zaidi katika eneo la kiungo ambalo Yanga imeongeza silaha za maana

Viungo Mohammed Abdallah 'Casemiro', Moussa Balla Conte, Mohamed Doumbia na Lassine Kouma wametua katika eneo hilo ambalo msimu uliopita Mudathir Yahya, Duke Abuya na Maxi Nzengeli walitamba wakati Stephane Aziz Ki na Khalid Aucho wakiondoka

Juzi katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya CHAN kati ya Tanzania dhidi ya Burkina Faso, Mudathir aliwaonyesha nyota hao wapya ni kwa kiasi gani wanakabiliwa na kazi kubwa kumnyan'ganya nafasi yake katika kikosi cha kwanza

Katika mchezo huo Mudathir alitumika kama kiungo namba 8, alihusika katika mabao yote mawili yaliyofungwa na Stars ambapo pasi yake kwa Clement Mzize ilipelekea mkwaju wa penati kabla ya kutoa pasi maridadi kwa Idd Nado aliyepiga krosi iliyojazwa kimiani na Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' anayesubiri utambulisho Yanga

Nafasi ya Duke Abuya nayo ni moto kwani kiungo huyo kutoka Kenya alimaliza msimu uliopita kibabe na pengine anaweza kuwa sababu ya Yanga kuachana na Aucho. Kwani Abuya yuko fit wakati wote, ni nadra kumuona akiwa nje kutokana na majeraha.

Maxi Nzengeli ni mchezaji mwingine kiraka ambaye sio rahisi kumuweka nje. Mara nyingi kabla ya msimu kuanza unaweza usiione nafasi ya Maxi kikosini lakini pale msimu unapoanza utamuona katika kikosi cha kwanza

Ni aina ya mchezaji ambaye kazi anayoifanya uwanjani hakuna kocha atakuwa tayari kumuweka nje pale anapokuwa fit

Kocha Romain Folz na benchi lake la ufundi watakuwa na kazi katika kuchagua wachezaji wa kuwatumia katika kila mechi

Kwani kila idala Yanga imesheheni wachezaji mahiri ambao wanaweza kutumika katika mchezo wowote

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’