Folz kuongezewa beki wa kati

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Aug 2025
Folz kuongezewa beki wa kati

Klabu ya Yanga SC inaendelea kufanya marekebisho ya kikosi chake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26, ambapo taarifa za ndani kutoka Jangwani zinadokeza kuwa mabingwa hao wa kihistoria wako mbioni kuongeza beki mwingine wa kigeni.

Hadi sasa, Yanga tayari imekamilisha usajili wa jumla ya wachezaji 12 wa kigeni, idadi ambayo ndiyo kikomo kinachoruhusiwa na kanuni za TFF kwa msimu. Hata hivyo, hali ya kiafya ya beki Yao Kouassi imekuwa changamoto inayowasukuma viongozi kufikiria kuongeza mchezaji mwingine katika eneo la ulinzi.

Yao alifanyiwa upasuaji wa goti mwezi Mei 2025, na kwa mujibu wa taarifa za kitabibu, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa hadi miezi sita. Ingawa kuna matumaini ya kupona mapema, uongozi wa Yanga hautaki kuhatarisha afya yake kwa kuharakisha kumrejesha uwanjani

“Hatujamtoa kwenye mipango ya muda mrefu, ndiyo maana tumemuongezea mkataba. Lakini kwa sasa tunatazama namna ya kumsajili beki mwingine ambaye atasaidia katika kipindi ambacho anaendelea kuimarika,” amesema mmoja wa maafisa waandamizi wa Yanga SC.

Kocha wa Yanga, Romain Folz, ameripotiwa kutoa mapendekezo maalum ya usajili wa beki wa kati, akisisitiza umuhimu wa kuwa na chaguo la haraka.

Ikumbukwe kwa sasa Yanga inawakosa mabeki wake tegemeo Ibrahim Bacca na Dickson Job ambao wako kwenye majukumu ya timu ya Taifa katika michuano ya CHAN

Hakuna uwezekano wa wachezaji walioko timu ya taifa kushiriki pre-season huku Yanga ikibaki na beki mmoja tu wa kati Bakari Nondo Mwamnyeto matarajio yakiwa kumtumia Aziz Andabwile kama beki wa  kati

Katika hatua nyingine, Yanga iko kwenye mazungumzo ya kuachana na winga wa DR Congo, Jonathan Ikangalombo, aliyejiunga na timu hiyo dirisha dogo la Januari 2025. Ingawa alirejea nchini kwa maandalizi ya msimu mpya, nafasi yake ni kama haipo tena baada ya Yanga kuongeza nyota watano wa kigeni.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’