Yanga kumkaribisha Ibenge Ngao ya Jamii

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
5 Aug 2025
Yanga kumkaribisha Ibenge Ngao ya Jamii

Bodi ya Ligi Tanzania imetangaza kalenda ya mashindano 2025/26 ambapo michuano ya Ngao ya Jamii itafungua pazia la msimu mpya.

Mabingwa watetezi Yanga wataungana na Simba, Azam na Singida Black Stars katika michuano hiyo kuanzia Septemba 11 hadi 14 mwaka huu.

Kwa mujibu wa kanuni katika mechi za nusu fainali Yanga, itakwaana na Azam FC, huku Simba ikiikabili Singida Black Stars

Ni kama marudio ya fainali ya msimu uliopita Yanga ikitwaa Ngao hiyo baada ya kuichapa Azam Fc mabao 4-1

Katika msimu huo Wananchi walicheza nusu fainali dhidi ya Simba iliyomaliza nafasi ya tatu na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0

Wakati huu Yanga inakutana tena na Azam Fc katika mchezo ambao utakutanisha makocha wapya katika ligi kuu

Romain Folz ataiongoza Yanga huku Florent Ibenge akiiongoza Azam Fc, bila shaka itakuwa mechi yenye hadhi ya fainali

Mshindi wa mchezo huo atatinga fainali ambapo Septemba 14 atachuana na mshindi kati ya Simba dhidi ya Singida Black Stars 

Yanga imeweka rekodi ya kibabe  katika michuano hiyo kwani kwenye misimu minne iliyopita imeshinda Ngao tatu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →