Klabu ya Yanga SC imetambulisha usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka Zoman FC, Celestin Ecua (23), ambaye msimu uliopita aliitumikia ASEC Mimosas kwa mkopo.
Hatimaye, ndoto ya mashabiki wa Yanga kuona nyota huyo akivaa jezi ya kijani na njano imekuwa halisi, leo akitambulishwa rasmi
Katika msimu wake wa mwisho akiwa ASEC Mimosas, Ecua alionyesha kiwango cha juu kwa kufunga mabao 15 na kutoa assists 12 katika michuano yote
Ni takwimu ambazo si tu zinaashiria uwezo wake wa kumalizia, bali pia ubunifu wake katika kutoa pasi za mabao.
Kinachomfanya kuwa lulu zaidi kwa Yanga ni uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi ndani ya uwanja. Ecua ni mchezaji anayetumia zaidi mguu wa kushoto, ana kasi, mbunifu, na mwenye uwezo wa kucheza kama winga wa pande zote au kiungo mshambuliaji namba 10.
Aina hii ya mchezaji huwapa makocha nafasi kubwa ya mbinu tofauti kulingana na mechi wanazokutana nazo.
Karibu Jangwani Ecua...!