Folz kuleta mbinu mpya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jul 2025
Folz kuleta mbinu mpya Yanga

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Ali Kamwe, amefunguka kuhusu dira mpya ya kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kamwe amesema usajili wa timu hiyo umezingatia mahitaji ya kimbinu ya kocha mpya Romain Folz, ambaye anakuja na mbinu mpya za kiuchezaji zinazolenga kubadilisha kabisa sura ya Yanga.

Katika maelezo yake, Kamwe amesisitiza kuwa viungo waliowasajili msimu huu wamechaguliwa mahsusi kwa uwezo wao wa kucheza nafasi nyingi uwanjani

“Viungo wote wa Yanga ukiwatazama msimu ujao, wanacheza popote katika eneo la kiungo. Muangalie Mudathir anaweza kucheza namba 6, 8 na hata 10. Hata Duke Abuya na Balla Conte, wote wana uwezo wa kucheza nafasi tofauti uwanjani,” amesema Kamwe.

Kamwe ametumia mfano wa gari na klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) kuelezea namna ambavyo Yanga itacheza msimu ujao:

“Umeshaona pistoni za gari zinavyofanya kazi, au umewaona PSG wanavyocheza katikati ya uwanja? Basi ndivyo Yanga tutakavyocheza msimu ujao,” aliongeza kwa kujiamini.

Ameeleza kuwa mfumo wa kocha Folz utahusisha mabadiliko ya mara kwa mara ya majukumu baina ya wachezaji uwanjani, hali itakayofanya Yanga kutotabirika.

“Kocha wetu analeta mfumo ambao wachezaji watakuwa wakibadilishana sana majukumu uwanjani, yaani kuna wakati kiungo mkabaji anaweza kuwa namba 10 na yule namba 10 akashuka chini kuwa mkabaji,” alisema kwa msisitizo.

Yanga inatarajiwa kuanza rasmi maandalizi ya pre-season mwishoni mwa wiki hii, huku wachezaji wake wakiendelea kuwasili jijini Dar es Salaam.

Kamwe amesema zoezi la utambulisho wa kikosi litakamilika ifikapo Julai 31, na kwamba timu hiyo itaelekea nchini Rwanda tarehe 13 Agosti kushiriki Rayon Sports Day, ambapo watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports kwenye Uwanja wa Amahoro tarehe 15 Agosti.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’