Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamethibitisha kumuongeza mkataba kiungo wao mshambuliaji Maxi Nzengeli
Maxi amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia katika mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam
Hii ni hatua muhimu kwa Yanga kuendelea kuwalinda nyota muhimu wa kikosi cha kwanza
Maxi ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa na tetesi nyingi katika dirisha hili huku taarifa mbalimbali zikidai hajasaini mkataba Yanga
Hata hivyo ni kama mabosi wa Yanga walikuwa wakiwaangalia tu wale waliokuwa wakizusha taarifa hizo kwani walishamalizana nae kitambo
Pacome Zouzoua, Duke Abuya, Mudathir Yahya na sasa Maxi wote wameongeza mikataba
Maana yake ni kuwa Yanga itaendelea kuwa imara katika safu yake ya kiungo na ushambuliaji kwani wachezaji hao walikuwa injini ya Yanga katika eneo la kiungo msimu uliopita